Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 December 2014
Thursday, December 04, 2014

Manchester United sasa ni mwendo wa Real Madrid.


Na Oscar Oscar Jr

Klabu ya Manchester United kwa sasa imejiandaa kufanya mambo kama ilivyo klabu ya Real Madrid. Baada ya kipindi cha usajili kilichopita kutumia Pauni 150M, sasa wamejipanga kuhakikisha wanawanasa wachezaji bora dunia kama wanavyofanya kwa sasa klabu ya Real Madrid.

Manchester wamejipanga kuvunja rekodi ya uhamisho msimu huu utakapokamilika huku kocha wa timu hiyo, Loius Van Gaal tayari akiorodhesha majina ya wachezaji ambao wanatarajiwa kutua Old Trafford. 

Yumo kiungo wa Roma, Kevin Strootman, ambaye atawagharimu si chini ya Pauni 30M, Mats Hummels Pauni 35M kutoka Borusssia Dotmund, Diego Godín, Pauni 25 kutoka Atletico Madrid.

Wengine wanaotua Old Trafford ni Dani Alves kutoka Barcelona kwa Pauni 15M, Arjen Roben kutoka Bayern Munich ambaye dau lake si chini ya Pauni 40M.

Endapo United watakubaliana na klabu ya Monaco ili kumnyakuwa Radamel Falcao kwa uhamisho wa kudumu, shambuliaji huyo atawagharimu Pauni 43.5M na kama watashindana, Van Gaal anataingia sokoni kutafuta mshambuliaji mwingine.

Bajeti ya Manchester United iliyotumika kwa misimu miwili itafikia dau la Pauni 350M baada ya msimu uliopita kutoa kitita cha Pauni 37.1M kwa Juan Mata na 27.5M kwa Marouan Fellain. 

Kabla ya msimu huu kuanza, Man United iliwaachia wachezaji 11 huku wengine tisa wakienda kwa mkopo na hii ni namna ambayo Van Gaal anataka kutengeneza timu yake huku akipandisha vijana sita kwenye kikosi cha kwanza kutoka timu B.

Nani, Tom Cleverley, Javier Hernández, Nick Powell, Reece James na Michael Keane, ni baadhi ya wachezaji waliopelekwa kwa mkopo klabu mbalimbali huku kukiwa hakuna uhakika kama watarejea msimu ujao na kujiunga na United.

Victor Valdes ambaye anafanya mazoezi na United kwa sasa huku akiendelea kupata matibabu, bado haijajulikana kama atajiunga na timu hiyo au laa.Valdes na Van Gaal wanajuana kwa kuwa, kocha huyo wa United alimfundisha soka kipa huyo wakati wote wako Barcelona.

David De Gea ambaye mkataba wake unamalizika 2015, bado mazungumzo ya mkataba mpya hayajaanza na kumekuwepo na tetesi za klabu ya Real Madrid kumuhitaji lakini United hawaonyeshi wasiwasi wowote na wanaamini kipa huyo atasaini mkataba mpya.

Klabu ilitarajia Phil Jones, Jonny Evans na Chris Smalling wangeweza kufanya vizuri hasa ukizingatia timu haina michuano ya Ulaya lakini majeruhi yamekwamisha malengo kwani wachezaji wote hao wamekuwa nje ya dimba kwa muda.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!