Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 December 2014
Monday, December 01, 2014

Roberto Soldado ageuka kuwa Shujaa wa Spurs.


Na Oscar Oscar Jr

Goli lililofungwa wa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Roberto Soldado liliwezesha timu ya Tottenham HotSpurs kuweza kujipatia alama tatu kwenye mchezo uliomalizika kwa Spurs kushinda bao 2-1 ndani ya dimba la White Hate Lane.

Soldado ambaye hajafunga goli lolote kwa Spurs tangu mwezi Machi, alifunga bao la ushindi na kurejesha amani kwenye kiti cha kocha Mouricio Pochettino ambaye alianza kuingia kwenye utata kufuatia matokeo mabovu.

Everton walijipatia bao la kwanza kupitia kwa mshambulia wa kimataifa wa Ubelgiji, Kelvin Millaras kabla ya Christian Eriksen kusawazisha na baadae Soldado kuitimisha ushindi huo wa tatu mfululizo kwenye michuano yote wanayoshiriki Tottenham Hotspurs msimu huu.

Bado mambo yanaonekana magumu kwa mshambuliaji wa Togo, Emmanuel Adebayor baada ya kuendelea kutupwa nje ya kikosi hicho huku washambuliaji Keane na Soldado wakionekana kupewa nafasi. 

Pamoja na kuwa goli la Soldado ni la tatu tangu ajiunge na timu hiyo akitokea klabu ya Valencia (ukiachilia mbali magoli aliyofunga kwa Penati), mashabiki wa timu hiyo ya London walionyesha kumshangilia sana shujaa wao wa mechi ya jana.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!