Roy Keane ameachia Ngazi Aston Villa.
Na Oscar Oscar Jr
Kocha msaidizi wa klabu ya Aston Villa, Roy Keane ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya Ireland ametangazwa na klabu yake, kujiondoa kwenye nafasi hiyo ili abaki na jukumu moja la kuiongoza timu ya taifa ya Ireland.
Roy Keane amekuwa kocha msaidizi wa kocha wa Aston Villa, Paul Lambert na kocha wa Ireland, Martin O’Neill. Kocha huyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa Manchester United, amesema kuwa kutimiza majukumu yote kwa klabu na taifa lake, umekuwa ni mzigo mzito.
Keane ameamua kuachia nafasi moja ili apate muda wa kutimiza majukumu yake vizuri na katika taarifa yake amenukuliwa akisema kuwa, haikuwa rahisi kutimiza majukumu yake kwa klabu na taifa kwa wakati mmoja.
Klabu ya Aston Villa imemkabidhi jukumu kocha Lambert kupendekeza mtu sahihi wa kuchukuwa jukumu la kocha msaidizi ndani ya kipindi kifupi kuanzia sasa.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na klabu, Keane ameonekana kumshukuru Paul Lambert kwa kumpatia ujuzi na kumpa uzoefu na ana amini atakuwa na fursa ya kusaidia taifa la Ireland.
0 comments:
Post a Comment