Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 December 2014
Wednesday, December 03, 2014

Chelsea hawa beep msimu huu.



Na Oscar Oscar Jr

Vijana wa kocha Jose Mourinho jana usiku waliendelea kuwasha moto mbele ya timu ya Tottenham Hotspurs kwenye dimba la Stanfford Bridge baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-0 huku Mkongwe, Didier Drogba akifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho kwa bao lingine.

Alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Eden Hazard aliyeweza kukata utepe baada ya kuiandikia Chelsea bao la kwanza baada ya kucheza "nipe-nikupe" na mkongwe, Drogba. 

Baaadaye, Drogba alifunga bao la pili kabla ya Loic Remy ambaye aliingia kipindi cha pili kufunga bao la tatu. Ushindi huu, umewafanya Chelsea kucheza mechi nne mfululizo bila kuruhusu nyavu zao kuguswa (Clean Sheets).

Matokeo haya yanawafanya Chelsea kubakia kileleni mwa msimamo huku wakiwa na pointi 36 na kuweka wigo wa  pointi sita kati yao  na Manchester City ambao wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 30 baaada ya ushindi wa 4-1 jana dhidi ya Sunderlan.

Spurs pengine wanapaswa kujilaumu baada ya kucheza vizuri hasa kipindi cha kwanza huku wakipoteza nafasi za wazi kabisa. Kocha Mouricio Pochettino aliamua kumuanzisha bwana mdogo, Harry Keane ambaye alipata nafasi mbili za wazi na kupoteza huku moja, mpira wake ukiishia kugonga mwamba wa goli na kurudi dimbani.

Ushindi huo wa jana unawafanya Chelsea kuwa timu ambayo haijapoteza mchezo kwenye mechi 23 za mashindano yote mfululizo. 

Spurs ambao hawajawahi kushinda Stanfford Bridge tangu mwaka 1990, walishindwa kwenda sambamba na kasi ya Hazard na nguvu za mtu mzima Didier Drogba.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!