Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 January 2015
Wednesday, January 28, 2015

Cameroon na Ivory Coast mbabe kujulikana leoNa Florence George

Michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) inazidi kushika kasi nchini Equatorial Guinea,ambapo mechi za mwisho za kundi D zinatarajiwa kuchezwa leo hii na kila timu ikiwa na nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.


Katika michezo miwili  ya awali katika kundi hilo yote ilimalizika kwa sare ya goli 1-1 kwa timu zote nne ,kwa maana hiyo timu za Cameroon,Guinea, Ivory Coast na Mali zote zina pointi mbili kila moja na mechi zao za mwisho ndio zitakazoamua timu zipi zitafuzu hatua ya robo fainali.

Cameroon itakuwa katika dimba la  Malabo kupambana na Ivory Coast huku Mali itakuwa katika dimba la  Mongomo kumenyana na Guinea na mechi zote zinatarajiwa kupigwa majira ya saa 21:00 hrs.

Cameroon na Ivory Coast zilitolewa mapema katika kombe la Dunia zilizofanyika mwaka 2014 nchini Brazil lakini zilikutana katika hatua ya kufuzu kombe hili ambalo katika mechi ya kwanza Cameroon iliibuka na ushindi wa goli 4-1 kabla ya kutoka sare katika mchezo wa pili.

Mali ambao walimaliza katika nafasi ya tatu  katika michuano miwili ya hivi karibuni ya AFCON watakuwa uwanjani kucheza na Guinea ambayo ililazimika kucheza michezo yao ya nyumbani ya  kufuzu nje ya nchi yao kutokana na ugonjwa wa Ebola lakini timu hiyo inaonekana kuimalika na kucheza kwa kujiamini na kujituma.

Katika michezo ya kundi C iliyochezwa jana iliisha kwa Ghana kushinda magoli 2-1 dhidi ya Afrika Kusini huku Algeria ikishinda magoli 2-0 dhidi ya Senegal,hivyo Ghana na Algeria zimeungana na timu za DR Congo,Tunisia,Equatorial Guinea.na Congo Brazzaville katika hatua ya robo fainali.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!