Na Chikoti Cico
Mshambuliaji wa timu ya Bastia inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa, Brandao amefungwa jela mwezi mmoja kwa kosa la kumpiga kichwa kiungo wa PSG Thiago Motta.
Tukio lilitokea mwezi wa nane kwenye mchezo kati ya PSG dhidi ya Bastia. Ingawa adhabu hiyo inaweza kugeuka kwa Brandao kufanya huduma kwa jamii kwa mwaka mmoja.
Mamlaka ya soka nchini Ufaransa tayari ilishamfungia Brandao kwa miezi sita kutojihusisha na soka na kulipa faini ya kiasi cha paundi 16000, wiki iliyopita shirikisho la soka nchini Ufaransa lilikataa rufaa ya mchezaji huyo dhidi ya adhabu ya kufungiwa huko kwa miezi sita.
Tukio la Brandao kumpiga kichwa Motta zilidakwa na camera za ulinzi za uwanja wa Parc De Princes, camera hizo zilimwonyesha Brandao akimsubiri Motta kwenye korido za vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo huo kabla ya kusogea karibu na Motta na kumpiga kichwa baada ya mchezo kati ya PSG dhidi ya Bastia hapo Agosti 16.
Mshambuliaji huyo kutoka Brazili amekuwa akihusika katika matukio mbalimbali ya ajabu uwanjani kwani msimu uliopita pia alifungiwa na shirikisho la soka nchini Ufaransa (FFF) ,kutokucheza michezo mitatu baada ya kumpiga kiwiko kiungo wa PSG Yohan Cabaye.
0 comments:
Post a Comment