Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 November 2014
Wednesday, November 26, 2014

Messi avunja rekodi Ulaya



Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi avunja na kuweka rekodi mpya ya magoli kwenye historia ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kufikisha jumla ya mgaoli 74 huku akimpita mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Raul Gonzalez aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo akiwa na magoli 71.

Hii ni rekodi ya pili kuvunjwa na Messi ndani ya siku tatu baada ya Jumapili iliyopita kuvunja rekodi nyingine ya magoli 251 ya Telmo Zarra kwa kufikisha jumla ya magoli 253 na kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye ligi kuu ya nchini Hispania maarufu kama “la liga”.

Messi alivunja rekodi hiyo kwa kufunga jumla ya magoli 3 kwenye ushindi wa Barcelona wa magoli 5-1 dhidi ya Sevilla.

Messi aliweza kuvunja rekodi hiyo ya ligi ya mabingwa Ulaya kwenye mechi dhidi ya APOEL Nicosia ambapo alifunga jumla ya magoli matatu kwenye ushindi wa Barcelona wa magoli 4-1.

Ushindi huo ulioweza kuifanya timu hiyo kufikisha alama 12 kwenye msimamo wa kundi F huku wakiwa wamepitwa kwa alama moja na PSG wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 13.

Baada ya kuvunja rekodi hiyo Messi akiongea na vyombo vya habari alisema “ Nina furaha kuvunja rekodi katika mashindano haya muhimu lakini huu ulikuwa mchezo mkubwa kwetu sote ukiweka rekodi kando, tunataka kushindana katika kila mashindano na tulihitaji alama usiku huu.

Akiongelea mechi ya mwisho kwenye msimamo wa kundi F dhidi ya PSG Messi alisema “ Tuna mchezo wa mwisho mgumu dhidi ya timu tunayoifahamu vizuri kwasababu tulicheza nao msimu uliopita na msimu huu pia lakini tupo nyumbani hivyo tuna nafasi nzuri ya kumaliza tukiongoza kundi”

Kwa kuvunja rekodi hiyo Messi anakuwa wa kwanza kwenye listi ya wafungaji bora wa muda wote kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya akiwa na magoli 74 katika michezo 91.

Raul Gonzalez akishika nafasi ya pili akiwa na magoli 71 katika michezo 142 huku Christiano Ronaldo akishika nafasi ya tatu akiwa na magoli 70 katika michezo 107 mpaka sasa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!