Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 January 2015
Sunday, January 25, 2015

Juma Pondamali zitazame upya Gloves za makipa wa Yanga.




Na Samuel Samuel
0652464525

Soka ni moja ya taaluma zinazo tegemea zaidi kipaji halisi, nguvu na kusimama imara katika mafundisho ya kila siku. Ili mchezaji adumu katika kiwango chake ni lazima azingatie miiko ya soka. 

Kuna nafasi ndani ya uwanja ambazo makocha huwa hawapendi kubadilisha wachezaji mara kwa mara hasa wanapokuwa tayari wamepata wachezaji ambao wanautendea haki mfumo na kiwango cha makosa ni kidogo. Nafasi hizo ni golikipa , kiungo wa chini pamoja na walinzi wa kati.

 Makosa aliyoyafanya Ali Mustafa " Batezi" mechi ya ligi dhidi ya Simba mwaka 2013 iliyomalizika kwa sare ya 3-3, yalimweka nje ya uwanja kwa zaidi ya mwaka mmoja mpaka hapo Mapinduzi Cup yalipokuja kukomboa kipaji chake na hiyo ilisababishwa na makosa ya kipa Deogratius Munishi katika mechi ya raundi ya tisa dhidi ya Azam FC iliyomalizika kwa sare ya 2-2. 

Deogratius aliruhusu goli rahisi sana kufungwa na John Bocco . Je kila kosa litakuwa linawaweka makipa wetu lock up mpaka hapo mmoja atakapokuja kukosa? Tazama Dida taratibu anapoteza namba national team kama ilivyokuwa kwa Mustafa. 

Hii sio sahihi, Juma Pondamali kama kocha wa makipa watengenezee ushindani magoli kipa wako kwa kuwabadilisha mara kwa mara kulingana na tension ya mechi na maandalizi stahiki ya mchezaji. 

Kwa sasa ni kama naona Dida amekwisha hukumiwa na yeye asubiri siku Mustafa akikosea atarudi uwanjani. Tunajali vipaji vyao? Makosa yapo , ni kiasi cha kuyasahihisha na kumrudisha mchezaji kwenye mchezo. 

Benchi la muda mrefu linaua kipaji cha mchezaji na saikolojia yake. Tubadili mfumo wa matumizi ya Gloves za makipa hao.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!