Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 December 2014
Thursday, December 04, 2014

Chelsea wataweza bila Nemanja Matic?


 Na Oscar Oscar Jr

Akiwa na umri wa miaka 21, kocha wa Chelsea wa wakati huo Carlo Ancelotti ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Real Madrid, alimsajili kiungo Nemanja Matic ingawa hakudumu na baadaye kuuzwa nchini Ureno kwenye klabu ya Benfica.

Pamoja na pasi nyingi za mwisho kutoka kwa Cesc Fabregas, pamoja na magoli mengi ya Diego Costa, bado kuna mtu anaitwa Nemanja matic ambaye anafanya timu ya Chelsea kuweza kuimarika hasa eneo la kiungo.

Matic amecheza dakika zote mechi za ligi kuu Uingereza msimu huu na tayari anashika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wachezaji waliopiga pasi nyingi msimu huu. 

Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure na fundi, Cesc Fabregas ndiyo waliopiga pasi nyingi kuliko Matic ambapo kila mmoja amepiga pasi 1,034 huku Matic akiwafuatia kwa kupiga pasi 840.

Diego Costa alikosekana kwenye ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Tottenham Hotspurs kutokana na kuwa na kadi tano za njano na sasa, Chelsea wanajiandaa kuwavaa Newcastle United bila kiungo Matic ambaye mchezo dhidi ya Spurs alipata kadi ya tano ya njano msimu huu na hivyo kumfanya atumikie adhabu ya kukosa mchezo mmoja.

John Obi Mikel ni moja ya wachezaji ambao wanatajwa kuchukuwa nafasi ya Matic kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Newcastle United ambao wanaonekana kuimarika licha ya kuwa na mwanzo mbaya wa ligi kuu.

 


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!