Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 November 2014
Wednesday, November 26, 2014

Liverpool yashikwa na Ludogorets.



Na Chikoti Cico

Hali bado haijatengamaa kwa timu ya Liverpool baada ya kuendelea kusuasua kwenye michuano mbalimbali huku ikitoka sare ya magoli 2-2- katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Vasil Leviski nchini Bulgaria.

Ludogorets walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Liverpool baada ya kupata goli kwenye dakika ya tatu ya mchezo kwa goli lililofungwa na Dani Abalo, kabla ya Rickie Lambert kuisawazishia Liverpool kwenye dakika ya nane ya mchezo, kiungo wa Liverpool Henderson aliifungia timu hiyo goli la pili kwenye dakika ya 37 ya mchezo.

Huku mpira ukielekea kuisha na Liverpool wakiamini wataondoka na alama tatu muhimu, kichwa kilichopigwa na Terziev na kujaa wavuni kwenye dakika ya 88 ya mchezo kilifanya ubao wa magoli kusomeka 2-2 baada ya filimbo ya kumaliza mchezo ya refa Antonio Miguel Mateu Lahoz kutoka Italia.

Matokeo hayo dhidi ya Ludogorets yanaifanya Liverpool kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi B huku wakiwa na alama nne tu baada ya kushinda mchezo mmoja, kutoka sare mchezo mmoja na kufungwa michezo mitatu kati ya michezo mitano waliyocheza ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Mpaka sasa Liverpool wamebakiza mchezo mmoja tu dhidi ya Basel wanaoshika nafasi ya tatu wakiwa na alama sita kwenye msimamo wa kundi B, Liverpool watahitajika kushinda mchezo huo ili kuvuka kuingia hatua ya mtoano, sare ama wakifungwa mchezo huo dhidi ya Basel utaifanya Liverpool kuaga michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!