TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Release N0.06
Februari,16/2015
Chama cha
kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimewapongeza wawakilishi wa Tanzania bara
katika michuano ya vilabu barani afrika klabu ya Azam FC na Yanga SC,kwa kuanza
na ushindi katika mechi zao za mkondo wa kwanza mwishoni mwa juma.
Yanga
walikuwa wa kwanza kuwapa raha watanzania siku ya jumamosi katika uwanjwa wa
taifa jijini,baada ya kuifunga mabao 2-0 timu ya maafande wa Polisi toka
Botswana BDF 11,mabao yete hayo yakitupiwa nyavuni na mshambuliaji Amis
Tambwe,ikiwa ni mchezo wa kuwania kombe la shirikisho.
Kwa upande
wa Azam FC,wao waliwafunga wababe wa soka huko Sudan klabu ya El-Merekh kwa
mabao 2-0 yaliyofungwa na Didier Kavumbagu pamoja na John Rafael Bocco,katika
mchezo wa kuwania kombe la klabu bingwa uliopigwa katika dimba la Azam Complex
Chamazi.
Mwenyekiti
wa DRFA,Almas Kasongo,amewapongeza wawakilishi hao wa Tanzania kwa hatua hiyo
nzuri waliyoanza nayo,na kusema kuwa maandalizi yaliyofanywa na vilabu hivyo
kuelekea mashindano hayo ya afrika,pamoja na ubora wa wachezaji na makocha,ni
dhahiri kwamba vitafanikiwa kuvuka katika hatua hiyo ya kwanza.
Kasongo,pia
amesema DRFA imeridhishwa na muitikio wa mashabiki wa Dar es salaam na maeneo
mengine nje ya jiji kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hizo mbili,na
kuwapongeza pia viongozi wa vilabu kwa matayarisho waliyoyafanya licha ya
dosari ndogo ndogo zilizojitokeza.
MICHUANO YA LIGI YA MKOA DAR
INAENDELEA.
Michuano ya
ligi ya mkoa wa Dar es salaam inaendelea tena wiki hii kwa timu 8 kushuka
katika viwanja tofauti,kupambana ili kuusaka ubingwa huo pamoja na kupata
nafasi ya kuingia katika ligi daraja la pili taifa.
Mechi za leo
Februari 16,2015/Azania Ngano watakipiga dhidi ya Yanga U20 (Katika uwanja wa
Karume),Stakishari watacheza na FFU (uwanja wa B.Mkapa),Changanyikeni wataumana
dhidi ya Tuamoyo (uwanja wa MWL/Nyerere) na New Kunduchi wataoneshana kazi
dhidi ya Sinza Stars (uwanja wa Kines).
Kivumbi hicho
kitaendelea tena kesho Kutwa Februari 18,2015 kwa Simba U20 kucheza na Ukonga
UTD (Uwanja wa karume),Red Coast watacheza dhidi ya Shababi
(MWL/Nyerere),Zakhem watacheza na Sifa UTD ( Uwanja wa Bandari) na
Beirahotspurs watakipiga dhidi ya Pan African (uwanja wa Kines).
IMETOLEWA NA DRFA
OMARY
KATANGA
Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Mawasiliano DRFA
0 comments:
Post a Comment