Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 December 2014
Saturday, December 27, 2014

Ronaldinho chupuchupu.


Na Chikoti Cico

Kiungo wa zamani wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Ronaldinho Gaucho aliyesajiliwa na timu ya Queretaro ya nchini Mexico mwezi Septemba mwaka huu ameponea chupuchupu kuachwa na timu hiyo inayoshirikia ligi ya nchini Mexico maarufu kama Clausura baada ya kuchelewa kuripoti kambini.

Raisi wa Queretaro, Joaquin Beltran alitangaza mapema wiki hii kwamba maisha ya Ronaldinho kwenye timu hiyo yatakuwa mashakani kama hataweza kuripoti klabuni hapo siku ya Ijumaa.

Ronaldinho ambaye amekosa mazoezi ya timu ya Quertaro maarufu kama Gallos Blancos kabla ya msimu wa mwaka 2015 kuanza yani “pre season” kwa wiki tatu anatarajiwa kufanyiwa vipimo siku ya Jumamosi kabla ya kuungana na wachezaji wengine wa timu hiyo ambao walianza mazoezi toka mapema mwezi Desemba.

Ronaldinho mwenye miaka 34 alicheza mara ya mwisho tarehe 23 ya mwezi Novemba mwaka huu huku akikabiliwa na matatizo ya kutokuwa fiti kwenye msimu wa kwanza wa ligi ya Mexico amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!