Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 December 2014
Sunday, December 07, 2014

Mapacha wampa kazi kocha wa Swansea City.



Na Chikoti Cico





Huku akiwa kocha mwenye umri mdogo zaidi kwenye ligi kuu nchini Uingereza kocha wa Swansea City Gary Monk akiwa na miaka 35 anapata wakati mgumu sana kuifanya kazi ya ukocha lakini pia kuwahudumia watoto wake mapacha Louis na Theo ambao wana umri wa miezi sita mpaka sasa.

Monk pia mwenye binti wa miaka mitatu aitwaye Remy alipewa kazi ya kuifundisha timu ya Swansea mwezi Februari kwa muda kabla ya kupewa mkataba wa moja kwa moja mwezi Mei mwaka huu akichukua nafasi ya kocha wa zamani wa timu hiyo mdachi 
Michael Laudrup.

Akiongelea changamoto hiyo ya kuwahudumia watoto hao mapacha wa kiume huku akitabasamu kocha huyo alisema “ni jinamizi, wote wanaumwa kwasasa na wanalalamika usiku wote na huwezi kuwaacha tu na kuacha walie hivyo itabidi uamke. Mke wangu (Alexandra) huamka zaidi kuliko mimi lakini bado unakuwa macho, si ndivyo?”

Aliendela kusema “ni ngumu, una watoto watatu,miaka mitatu na chini ya hapo na hatujatapa familia ya karibu kwa maana ya kutusaidia, sio kama unaweza kumpigia mtu simu na kumleta awepo. Mke wangu amefanya vyema sana. Ni wazi huwa najaribu kutafuta muda kutumia nao kwasababu ni muhimu kujaribu kuwa na muda na kutumia na familia. Lakini pia kuna familia nyingine ambayo ipo hapa, watoto 25”

Wakati huo huo kocha huyo ana kazi nyingine ngumu zaidi kuwaongoza watoto 25 wa Swansea kushinda mchezo mwingine wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya West ham utakaopigwa kwenye uwanja wa Upton Park ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ndani ya msimamo wa ligi hiyo, kwasasa Swansea inashika nafasi ya nane ikiwa na alama 22.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!