Na Chikoti Cico
.
Kipa
wa Manchester City na timu ya taifa ya Uingereza Joe Hart anatarajia
kupewa mkataba mpya wa miaka minne na nusu na timu hiyo kutoka jiji la
Manchester kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya AS Roma
utakaopigwa siku ya Jumatano nchini Italia.
Hart ambaye kwasasa anapokea mshahara wa kiasi ya pauni 80,000 kwa wiki anatarajia kuongezewa mshahara huo na kufikia pauni 165,000 kwa wiki na kuwa moja ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa ndani ya timu ya Manchester City, mshahara huo utajumuisha bonasi na haki ya taswira yake.
Kipa huyo aliyesajiliwa na City mwaka 2006 akitokea timu ya Shrewsbury kwa ada ya pauni 60,000 na mpaka sasa ameweza kunyakua makombe mawili ya ligi ya Uingereza na kombe la FA huku pia akiwa kipa chaguo la kwanza kwenye timu ya taifa ya Uingereza.
Mkataba huo mpya utamfunga Hart mpaka mwaka 2019 kuichezea City ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza ikiwa na alama 33 katika michezo 15 iliyocheza ikipitwa na vinara Chelsea kwa alama tatu.

0 comments:
Post a Comment