Searching...
Image and video hosting by TinyPic
14 September 2014
Sunday, September 14, 2014

Muunganiko wa Lionel Messi na Neymar umeanza kuzaa matunda


  Na Oscar Oscar Jr

Mshambuliaji bora kwa sasa wa Brazil, Neymar, alitoka benchi na kufunga magoli yote mawili yaliowewazesha wababe wa Hispania, Barcelona, kujipatia ushindi wa tatu mfululizo kwa kuinyuka Athletic Bilbao 2-0 kwenye ligi kuu ya Hispania, La Liga hapo jana. 

Muunganiko wa Lionel Messi na Neymar umeanza kuzaa matunda sasa baada ya wawili hao kutofanya vizuri msimu uliopita. 
"Mafahari" hao waliwachanganya wachambuzi wengi wa soka na wengi hawakutoa nafasi kwa wawili hao kung'aa pindi wanapocheza pamoja na kuzaa matunda. Alikuwa ni Lionel Messi ambaye alimtengenezea Neymar mabao yote mawili ya mchezo.

Wakati Barcelona wakianza vema, wapinzani wao Real Madrid walijikuta katika hali ngumu baada ya kujikuta wakichezea kichapo cha mabao 2-1 mbele ya watani wao wa jadi Atletico Madrid ndani ya dimba la Santiago Bernabeu. 

Biashara ya kuwauza kiungo mkabaji Xaib Alonso aliyetimkia klabu ya Bayern Munich na kiungo mshambuliaji Angel Di Maria aliyejiunga na Manchester United, bado kunaendelea kuitesa klabu ya Real Madrid.

Safu ya kiungo ya Real Madrid kwa sasa inaongozwa na Ton Kroos, Luke Modric na James Rodriguez ambao kiasilia, hakuna kiungo mkabaji kati yao. 

Kutokuwepo kwa Semi Khedira ni pengo kubwa kwa watoto wa kocha Carlo Ancieloti na mambo yakiendelea kwenda kombo, kuna uwezekano bosi huyo raia wa Italia akakalia kuti kavu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!