Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 January 2015
Saturday, January 10, 2015

Kocha mpya wa Barcelona amenukia.


Na Oscar Oscar Jr

Kuna kila dalili za kocha mkuu wa Barcelona, Luiz Enrique kutimuliwa ndani ya siku za hivi karibuni kutokana na kutoelewana na baadhi ya wachezaji ambao ni mastaa kwenye timu hiyo akiwamo Lionel Messi.

Rais wa Barcelona, Josep Bartomeu anadaiwa kufanya mazungumzo ya siri na mshambuliaji Lionel Messi na tayari kuna majina mawili yamependekezwa ya kuja kuchukuwa nafasi ya Luiz Enrique.

Kocha wa Brighton, Oscar Garcia ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa timu hiyo na kocha wa timu ya vijana U-19, hivi karibuni alitajwa kuchukuwa nafasi ya kuwa mkurugenzi wa ufundi wa Barcelona baada ya Andoni Zubizarreta kufutwa kazi.

Garcia aliikataa nafasi hiyo na kudai kuwa, ndoto yake kwa sasa ni kuwa kocha na sio mkurugenzi. Garcia aliwaongoza vijana wa U-19 wa Barcelona kushinda mataji matatu mwaka 2011.

Katika sakata hilo, aliyewahi kuwa kocha wa Barcelona, Frank Rijkaard naye yuko mbioni kurejea Camp Nou kuinoa timu hiyo baada ya kufanya kazi hapo awali kwa mafanikio zaidi na Messi ameonekana kumkubali mkufunzi huyo.

Luiz Enrique ambaye ameiongoza Barcelona kwenye mechi  17 za La Liga, amefanikiwa kushinda mechi 12, kutoka sare kwenye mechi mbili na kupoteza mechi tatu huku timu ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu. 

Barcelona bado inashiriki kwenye michuano yote mitatu huku wakitinga kwenye hatua ya 16 bora klabu bingwa Ulaya. Katika sakata hili, Lionel Messi ameonekana kupewa nafasi kubwa sana kuamua hatima ya kocha Luiz Enrique na leo wako dimbani dhidi ya Atletico Madrid.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!