Na Chikoti Cico
Kipa wa zamani wa klabu ya Barcelona Victor Valdes ambaye kwa muda wa miezi mitatu amekuwa akifanya mazoezi na timu ya Manchester United katika kujiweka fiti baada ya kuumia, amesaini mkataba wa kuichezea timu hiyo kwa miezi 18 na kuna uwezekano wa kuongezewa muda huo.
Akiongea na vyombo vya habari baada ya kusaini mkataba huo Valdes alisema “ni heshima sana kusaini kwaajili ya Manchester United, ningependa kumshukuru Louis van Gaal na klabu kwa kuniruhusu mimi kufanya ukarabati wa afya na kufanya mazoezi na timu hapa Aon Training Complex”.
Aliendelea kusema “kwa muda mfupi hapa, naweza kuona hii ni klabu ya kipekee, nilifanya kazi na Louis van Gaal wakati wa muda wangu na Barcelona FC na kupata nafasi ya kufanya nae kazi hapa Manchester United ni ndoto kutimia”.
Nae kocha wa Manchester United Louis van Gaal baada ya kukamilisha usajili huo wa kwanza kwa klabu hiyo katika dirisha hili dogo la usajili alisema “ninafuraha Victor amesaini kwaajili ya klabu,Victor ni kipa mwenye uzoefu na rekodi zake zinazungumza zenyewe, nimesema mara nyingi kwamba Manchester United mara zote itavutiwa na wachezaji bora”
Aliendelea kumzungumzia Valdez akisema “Victor amebaki mweledi wakati wote wa ukarabati wa afya yake kutokana na majeruhi na amekuwa akivutia wakati wa mazoezi na kikosi cha kwanza kwa wiki zilizopita, amejiunga na klabu kama kipa namba mbili na ni ongezeko zuri kwa kikosi cha kwanza”
Valdez ambaye alikuwa mchezaji huru toka alipoachwa na klabu ya Barcelona kwenye majira ya joto ya mwaka uliopita anatarajiwa kutoa changamoto kwa kipa namba moja wa United David de Degea.
0 comments:
Post a Comment