Tambwe kuisanbaratisha Yanga Jumamosi hii?
Na Samuel Samuel
Kuelekea pambano la watani wa jadi jumamosi hii, Simba wana injini ya magoli toka Burundi, Hamis Tambwe. Toka amejiunga na Simba ameonesha uwezo mkubwa wa kufunga magoli kama mshambuliaji wa kati.
Kiufundi Hamisi Tambwe ni aina ya washambuliaji ambao ni wamaliziaji wazuri wa kazi zinazosukwa aidha na winga wa kulia au kushoto na hata viungo wa kati.
Amekuwa mfungaji mzuri si kwa klabu yake ya Simba tu hata timu ya taifa ya Burundi wana mtegemea katika kuwapatia magoli.
Wakati Tanzania ikisheherekea sikukuu ya Muungano mwaka huu, jioni ilichezwa mechi kati ya Taifa Stars na Burundi. Tanzania ili lala 3-0 huku magoli mawili yakifungwa na Hamisi Tambwe na Didier Kavumbagu akifunga moja.
Katika soka kuna washambuliaji wa kati wa aina mbili, wapo wenye asili ya kiungo mchezeshaji( play makers) .
Hawa wana uwezo mzuri wa kutafuta mipira , kukaba na hata kuwatengenezea assist wachezaji wengine waliopo katika nafasi nzuri za kufunga.
Na mara nyingi wanakuwa wazuri kwenye mfumo wa 4-3-3 au 4-3-1-2. Aina ya pili ni wamaliziaji wa kazi za viungo na mawinga.
Wana uwezo mzuri wa kukaa kwenye njia ya mpira na kufunga magoli.
Sasa back line ya Yanga lazima ikae macho inakutana na Hamisi Tambwe mwenye mzuri wa kujiweka kwenye njia na kufunga magoli mazuri maana ana uwezo mzuri wa kutumia nafasi.
Msimu uliopita aliibuka mfugaji bora wa VPL kwa kutupia magoli 19 kwenye kamba kwa style tofauti. Alifunga magoli hayo kwa penati na hat tricks. Tambwe anahitaji kupangiwa viungo wenye kasi na uwezo wa kutoa pasi za mwisho.
Kama kulia akipangwa Ndemla , Kushoto Okwi au Singano na kiungo cha mbele akawekwa Amri Kiemba basi Nadir , Yondani , Joshua , Abdul na Dida wana kazi ya ziada kumzuia mnyama huyu asicheke na nyavu.
0 comments:
Post a Comment