Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 January 2015
Wednesday, January 07, 2015

Wachezaji 12 wapigwa chini na Ghana AFCON 2015.


Na Chikoti Cico

Ghana yatangaza kikosi cha mwisho. Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Avram Grant ametangaza kikosi cha mwisho cha timu hiyo kuelekea michuano ya kombe la mataifa ya Afrika yatakayoanza tarehe 17 Januari nchini Equatorial Guinea. 

Katika kikosi hicho cha mwisho Grant amewaacha Jeffrey Schlupp anayichezea Leicester City na Samuel Inkoom anayekipiga kwenye klabu ya Houston Dynamo huku pia akiwaacha wachezaji 12 walioshiriki fainali za mataifa ya Afrika zilizofanyika nchini Afrika ya Kusini miaka miwili iliyopita. 

Ghana wako kundi C pamoja na timu za Algeria, Senegal na Afrika ya Kusini na mchezo wa kwanza watacheza Januari 19 na Senegal. Kikosi kamili cha wachezaji 23 ni: 

Makipa: Razak Braimah (Mirandes, Spain), Fatau Dauda (AshGold) and Ernest Sowah (Don Bosco, DR Congo). 

Walinzi: Harrison Afful (Esperance, Tunisia), John Boye (Erciyesspor, Turkey), Jonathan Mensah (Evian, France), Mohammed Awal (Maritzburg, South Africa), Baba Rahman (Augsburg, Germany), Edwin Gyimah (Mpumalanga Black Aces, South Africa), Daniel Amartey (Copenhagen, Denmark). 

Viungo: Mohammed Rabiu (Krasnodar, Russia), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italy), Afriyie Acquah (Parma, Italy), Solomon Asante (T.P. Mazembe, DR Congo).

Wengine ni Christian Atsu (Everton, England), Mubarak Wakaso (Celtic, Scotland), Andre Ayew (Olympique Marseille, France), Frank Acheampong (Anderlecht, Belgium), David Accam (Chicago Fire, USA). 

Washambuliaji: Jordan Ayew (Lorient, France), Mahatma Otoo (Songdal, Norway) Asamoah Gyan (Al Ain, UAE), Kwesi Appiah (Cambridge United, England).

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!