Na Chikoti Cico.
Huku mchakato wa kupatikana kwa mchezaji bora wa dunia kunyakuwa tuzo ya Ballon d’Or ukiendelea kuteka hisia za wadau wa soka, mchezaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo aendelea kujitengenezea mazingira mazuri baada ya jana usiku kuipatia ushindi Madrid dhidi ya Celta Vigo kwa kufunga magoli matatu (hat trick).
Magoli hayo matatu yamefanya Ronaldo kufikisha jumla ya magoli 200 kwenye mechi 178 alizoichezea Madrid katika mashindano mbalimbali huku pia akiisaidia timu hiyo kuendelea kujikita kileleni mwa la liga kwa kufikisha alama 36 katika michezo 14 waliyocheza msimu huu.
Pia Ronaldo amevunja rekodi ya “hat trick” 22 zilizofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Madrid, Alfredo di Stefano kwa kufikisha jumla ya “hat trick” 23 kwenye ligi hiyo hivyo kumpita mpinzani wake mkubwa kwenye tuzo ya Ballon d’Or, Lionel Messi mwenye “hat trick 20”.
Wakati Ronaldo akifikisha jumla ya magoli 23 baada ya jana kufunga magili matatu dhidi ya Celta Vigo, ushindi huo umeiwezesha klabu ya Madrid kufikia rekodi iliyowekwa na Frank Rijkaard wakati akiifundisha Barcelona kwenye msimu wa 2005-06 kwa kushinda michezo 18 mfululizo.
0 comments:
Post a Comment