Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 November 2014
Sunday, November 16, 2014

Mohamed Traore kutua Azam Fc


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kumnasa beki wa kati Pascal Wawa ambaye alikuwa anakipiga na klabu ya El-Merreikh, sasa habari mpya ni kuwa mabingwa hao wa ligi kuu msimu uliopita wanajipanga kumnasa mshambuliaji mwingine kutoka klabu hiyo, Mohamed Traore.

Traore ambaye ni raia wa Mali anadaiwa kuja kujiunga na wanalamba lamba mwishoni mwa mwezi huu. 

Azam baada ya kupata ubingwa wa ligi kuu, ndoto zao ni kuona wanafanikiwa kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika na ndiyo maana wanaonekana kusaka wachezaji kutoka kila kona ya Afrika.

Traore kwa sasa yupo kwenye timu ya Taifa ya mali ambayo inajiandaa na mchezo dhidi ya Algeria wa kutafuta nafasi ya kufuzu kwa michuano ya bara la Afrika ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi hapo mwakani kwenye viwanja vya Guinea ya Ikweta.

Kwa usajili hao ni wazi kuwa, mshambuliaji raia wa Haiti, Lionel Saint Preux na Mmali, Ismail Diara wataonyweshwa mlango wa kutokea. 

Azam itakuwa na wachezaji wa kigeni watano ambao ni Kipre Thetche, Kipre Balou, Didier Kavumbagu, Pascal Wawa na Traore.

Azam kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kujikusanyia pointi 13 sambamba na timu ya Yanga ambayo inashika nafasi ya pili huku Mtibwa Sugar wakiongoza ligi hiyo wakiwa na alama 15. Mechi inayofuata ya ligi kuu ni kati ya Yanga dhidi ya Azam.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!