FIFA yampiga STOP Hatem Ben Arfa
Na Florence George
Taarifa kutoka Shirikisho la soka la nchini Ufaransa(FFF) zinasema kuwa shirikisho la soka Duniani FIFA limekataa kutoa ruhusa kwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Hatem Ben Arfa kucheza katika katika ligi kuu nchini Ufaransa.
Mchezaji huyo alijiunga na Nice mapema mwezi huu akitokea katika timu ya Newcastle United ya nchini Uingereza na atalazimika kusubiri hadi msimu ujao ili aweze kukipiga katika timu hiyo.
FFF wanasema kuwa FIFA imegoma kumsajili Ben Arfa kama mchezaji wa Nice kutokana na mchezaji huyo kuwa tayari ameshachezea timu mbili msimu huu ambazo ni Newcastle United na Hull City.
Ben Arfa alijiunga na Newcastle United mwaka 2010 akitokea timu ya Marseille ya nchini Ufaransa ambapo alijikuta akipoteza namba siku za hivi karibuni kwa kocha aliyekuwa anakinoa kikosi hicho Alan Pardew ambaye ametimkia katika klabu ya Crystal Palace.
Katika msimu huu Ben Arfa ameichezea timu ya Newcastle katika mechi chini ya miaka 21mwezi August kabla ya kutolewa kwa mkopo katika klabu ya Hull City ambapo hata huko alishindwa kuonyesha uwezo hali i9liyopelekea kutemwa na kocha Steve Bruce.
0 comments:
Post a Comment