Timu yetu ya Taifa inapigana kila siku kwa nguvu moja,ari na kila kitu
kutuwakilisha.Unapoanza kuichukia Taifa Stars eti kwa sababu imefungwa
ni "immaturity" katika soka.
Tunatamani tucheze na kufanikiwa
kama Hispania,Ujerumani n.k lakini bado hatuna uwezo huo.Kuna magumu
mengi wachezaji wetu wanakutana nayo hasa wanapokuwa nje ya nchi,kwa
taarifa yako,hakuna timu Duniani ambayo haifungwi.
Tusikubali
kuwa watumwa wa kina Falcao,marco Reus na Hummels kila siku,Tuna kina
Samatta,Kiemba na Yondani ambao wanatugusa zaidi ya hao wengine ingawa
tunakubali wametuzidi uwezo.
Hapa tulipo leo tumepiga hatua,ukichunguza Stars ya kabla ya Maximo,ya maximo na hii ya leo utagundua kwamba tunasonga mbele.
Bado tunanafasi ya kwenda BRAZIL 2014 hata kama ni finyu ipo.mimi na stars wote ni #made in Tanzania.
0 comments:
Post a Comment