Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 January 2015
Friday, January 02, 2015

Bayern yanasa kifaa kipya





Na Florence George

Mabingwa wa soka nchini Ujerumani klabu ya soka ya Bayern Munich imetangaza kumsajili  mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani, Joshua Kimmich kutoka timu ya VfB Stuttgart kwa kiwango cha pesa ambacho hakikuwekwa wazi.

Mchezaji huyo atajiunga na mabingwa hao katika kipindi cha joto mwaka huu pale mkataba wake wa mkopo katika klabu RB Leipzig utakapomalizika.

Inaripotiwa kuwa Kimmich mwenye umri wa miaka 19, amesaini mkataba wa kuitumia timu hiyo hadi mwaka 2020 na inasemekana kuwa ndiye mchezaji aliyekuwa anawindwa sana na kocha wa timu hiyo Pep Guardiola.

Guardiola ameamua kumsajili mchezaji kutokana na viungo wake wakabaji kama Thiago Alcantara kuwa majeruhi huku umri kwa wachezaji kama Xabi Alonso na Bastian Schweinsteiger ukionekana kuwatupa mkono.

Kiungo huyo mkabaji hajaichezea hata mechi moja timu ya VfB Stuttgart lakini ameshacheza michezo 13 hadi sasa katika timu ya RB Leipzig inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo.

Joshua Kimmich amefanikiwa kuchezea katika vikosi vyote vya timu ya taifa ya Ujerumani kwani amecheza katika timu chini ya umri wa miaka 15 hadi 21 huku akiwa sehemu wa wachezaji walioweza kuipa ubingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Ujerumani chini ya miaka 19 mwezi July mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!