Na Oscar Oscar Jr
Mechi mbalimbali zimepigwa siku ya Jumapili Usiku kufuzu kwa kombe la Euro huku timu ya taifa ya Uholanzi ikigawa dozi kwa kuitandika Latvia kwa bao 6-0.
Mabao ya Uholanzi yalifungwa na Klaas Juan Huntelaar aliyefunga mawili huku Arjen Roben, Roben Van Persie na Jeffrey Bruma wakikamilisha idadi hiy ya magoli.
Katika mchezo huo, tukio baya ilikuwa ni kuumia kwa kiungo mkabaji wa Manchester United, Delay Blind na kutolewa kwenye dakika ya 20. Habari hizi sio nzuri kwa kocha wa Loius Van Gaal ambaye mwishoni mwa juma hili atacheza dhidi ya Arsenal.
Kwa upande mwingine, mabingwa watetezi wa kombe hilo la Euro, timu ya taifa ya Hispania imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Belarus huku kiungo wa Real Madrid, Isco akiwa mmoja wa wafungaji wa magoli hayo. Uwezo anaouonyesha Isco kwa sasa, unazidi kumuweka Gareth Bale kwenye wakati mgumu sana.
Timu ya taifa ya Wales nayo imetoka sare ya bila kufunga na timu ya Ubelgiji huku timu hizo zikitawala mchezo kwa kupokezana. Wales walionekana kufanya vizuri sana hasa kipindi cha kwanza ambapo, mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale alikuwa mwiba kwa Ubelgiji.
Kipa wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji, Thibout Courtois aliendelea kuwa kwenye ubora wake na kuokoa michomo mingi. Ubelgiji walikuja kipindi cha pili wakiwa moto lakini bado milango ya timu zote iliendelea kwa migumu.
0 comments:
Post a Comment