Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 January 2015
Tuesday, January 13, 2015

Sina tatizo na kocha Manuel Pellegrini








Na Florence George

Beki wa kimataifa wa Serbia Matija Nastasic atajiunga kwa mkopo na timu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani kama atafanikiwa kufaulu vipimo vya Afya vya timu hiyo winavyotarajiwa kufanyika wiki hii huko Doha ambapo timu hiyo imeweka kambi.

Beki huyo amekuwa hapati namba katika timu ya Manchester City tangu alipowasili kocha Manuel Pellegrini huku hadi sasa akiwa amecheza mechi moja tu ambayo ilikuwa ni ya ngao ya jamii dhidi ya Arsenal mapema mwezi August mwaka jana.

Akiulizwa swali kama anatatizo lolote na kocha Pellegrini ,Nastasic alisema kuwa hana tatizo lolote na kocha huyo bali amekuwa na kipindi kigumu kwani ndani ya miezi sita ya hivi karibuni hajacheza mechi yoyote ile ya ligi kuu.

Aliendelea kusema kuwa ameamua kwenda huko ili aweze kucheza mechi nyingi na amependelea kwenda Ujerumani baada ya kuongea na kocha wa timu hiyo Roberto Di Matteo japokuwa kulikuwa na timu nyingine kutoka Uingereza zilizokuwa zinamuhitaji.

Kama akifanikiwa kufaulu vipimo vya afya, Nastasic atakuwepo katika kikosi cha Schalke 04 kitakachopambana na Real Madrid katika hatua ya 16 bora katikati ya mwezi wa February huku akimaliza kwa kuwatakia kila la kheri timu ya Manchester City katika mashindano yao wanayoshiriki.











0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!