Na Chikoti Cico
Baada
ya kumalizika mechi ya Ligi kuu ya Uingereza kati ya Manchester United dhidi ya
Chelsea iliyopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford ambapo mechi iliisha
kwa matokeo ya sare ya 1-1, Loius Van Gaal, kocha wa Man United amekasirishwa na Nahodha wake Robin Van Persie.
Manchester United wakisawazisha goli kwenye dakika ya 94 kupitia kwa Robin Van Persie, kocha wa Manchester United Luis Van Gaal hakupendezwa na shangilia ya Van Persie ya kuvua jezi na kuirusha juu kitendo alichokiita kuwa ni cha kipumbavu.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo Van Gaal aliisifu timu yake kwa kusema “ Chelsea walijaribu kuumaliza mchezo walifanya uwanja uwe mkubwa na ilitufanya tukimbie sana ila tulipigana mpaka mwisho.
Tulistahili wakati tulipofunga, tulitengeneza nafasi nyingi zaidi kuliko Cheslea”
Kocha huyo mdachi aliendelea kusema “Chelsea walitengeneza nafasi nafasi moja kipindi cha kwanza lakini ni kukosekana kwa mawasiliano kulikopeleka goli lao, baada ya Chelsea kufunga tulichanganyikiwa ila tulicheza vizuri sana”
Katika mchezo huo Chelsea waliweza kupata goli dakika ya 53 kupitia kwa Didier Drogba baada ya kuunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Fabregas.
Akiongelea kitendo cha Van Persie kuvua jezi wakati akishangilia goli la kusawazisha alisema “Kilikuwa ni kitendo cha kipuuzi, naona alikuwa na furaha lakini alipewa kadi ya njano sio uerevu sana”
Kabla ya goli hilo kufungwa Chelsea walimpoteza beki Ivanovic baada ya kuonyesha kadi ya pili ya njano hivyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumwangusha Angel Di Maria.

0 comments:
Post a Comment