Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 October 2014
Sunday, October 26, 2014

Martin Skrtel amsikitikia Balotelli.


Na Chikoti Cico


Beki wa Liverpoo, Martin Skrtel amsikitikia mchezaji mwenzake wa Mario Balotelli ambaye mpaka sasa amefunga goli moja tu kati ya mechi 11 alizoichezea Liverpool toka aliposajiliwa kwa paundi milioni 16 kutoka AC Milan mapema mwezi wa nane huku pia akikosa magoli ya wazi kwenye mechi nyingi alizocheza.

Balotelli ambaye karibuni aliingia kwenye mzozo na kocha wa Liverpool Brendan Rodgers kwa kitendo chake cha kubadilishana jezi na mchezaji wa Real Madrid Pepe kabla ya mpira kuisha amekuwa na mwanzo mgumu kwenye timu ya Liverpool hasa kipindi hiki ambacho mshambuliaji mwenzake wa Liverpool Daniel Sturridge akiwa majeruhi.

Skrtel akimzungumzia Balotelli baada ya mechi dhidi ya Hull City alisema “ Anafanya jitihada kubwa na anaonyesha wakati mzuri uwanjani, namsikitikia anafanya juhudi kubwa mazoezini na kwenye mechi ila hajapata magoli. Tuna imani nae na tutamuunga mkono tukitumai ataanza kufunga magoli”

Liverpool waliotoka sare ya 0-0 dhidi ya Hull City kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyopigwa kwenye uwanja wa Anfield siku ya Jumamosi mpaka sasa wanashika nafasi ya saba wakiwa na alama 14 kwenye msimamo wa ligi huku mpaka sasa wakiwa wameshinda michezo minne na kupoteza michezo mitatu na kutoka sare michezo miwili kati ya michezo tisa waliocheza kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Skrtel baada ya kumzungumzia Balotelli pia alizungumzia mchezo wa Liverpool dhidi ya Liverpool akisema “Ni kawaida sehemu ya ulinzi inapofungwa kipa anakuwa wa kwanza kulalamikiwa, tumelirekebisha hilo nyavu zetu hazikutikiswa (clean sheet) lakini hatukupata alama tatu hivyo hiyo haitoshi. 


Tulicheza kwaajili ya alama tungeweza kushinda inaumiza” aliendelea kusema “ningetamani kushinda 5-4 na kupata alama tatu kuliko sare ya 0-0 na kupata alama moja, nafikiri tulicheza vizuri basi tu hatukuweza kufunga goli”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!