Mbeya City wakutana na beki uchochoro VPL.
Na Samuel Samuel.
0652464525
Ndanda Fc kutokana mkoani Mtwara ambayo imepanda ligi kuu msimu huu sambamba na Polisi Moro na Stand United ndiyo timu yenye safu ya ulinzi uchochoro msimu huu.
Mechi yao ya kwanza walianza kwa mkwara mzito baada ya kuibamiza 4-1 wageni wenzao wa ligi Stand United tena katika dimba lao la ugenini pale Kambarage.
Matokeo yale yaliwashitua wengi hasa kocha wa timu hiyo ambaye kwa sasa amegeuka kocha msaidizi kwa kumpisha kocha toka nchini Uganda.
Ukiangalia msimamo wa ligi timu hiyo imeshinda mechi mbili tu kati ya saba iliyocheza lakini mechi ya pili ikiwatikisa 1-0 mabingwa watetezi wa ligi hiyo Azam FC.
Ndanda kama inataka kubaki ligi kuu ni lazima iimarisha safu yake ya ulinzi hasa mabeki wa kati. Mpaka ina maliza mzunguko wa saba wa ligi kuu, Ndanda imeruhusu nyavu zake mara kufungwa mabao 12.
Ukiitazama safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ina magoli saba si tofauti kubwa sana na kinara wa ligi hiyo mwenye magoli 10. Kwa sasa baada ya kumnasa kiungo mkabaji Omega Seme, basi kuna uwezekano mkubwa kwa timu hiyo kubadilika katika ukabaji na ushambuliaji na kesho watakuwa ugenini kuwakabili mbeya City kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya
0 comments:
Post a Comment