Na Chikoti Cico
Baada
ya Christiano Ronaldo kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu nchini
Hispania maarufu kama la liga na kumpita Lionel Messi, mchezaji wa
Barcelona Javier Mascherano naye pia ampita Messi na kunyakua tuzo ya
mchezaji bora wa msimu wa 2013/2014 kwa timu ya Barcelona, Messi amewai
kuchukua tuzo hiyo mara tatu katika miaka minne iliyopita.
Mascherano ambaye amekuwa akicheza kama beki wa katikati na wakati mwingine kama kiungo mkabaji kwa sehemu kubwa ya msimu uliopita akiongea na mtandao wa Barcelona baada ya kunyakua tuzo hiyo alisema
“ Nawashukuru ninyi nyote mlionipigia kura kupokea tuzo hii, tutajitahidi kuendelea kufanya mambo kama ambavyo tunafanya mpaka sasa, kwa kujitolea kule kule huku tukijaribu kubaki na imani kwa kile kinachohitajika na klabu kama hii ambacho ni kikubwa”
Tuzo hii hutolewa baada ya mchezaji kupigiwa kura na wapiga kura wanaohusika kwa timu ya Barcelona ni wanachama maalum kutoka chombo cha habari toka Catalan pia maofisa wakuu wa klabu huku Raisi wa Barcelona Josep Maria Bartomeu akiwa mmojawapo.
Baada ya kutoa tuzo hiyo Raisi wa Barcelona Josep Maria Bartomeu alisema “ Nilikuwa sehemu ya chombo kilichohusika kumchagua Javier Mascherano.
Nahitaji kukwambia Javier, kulikuwa na malumbano mwanzoni lakini baada ya jina lako kutokea, majibu yalikuwa ya kufanana hivyo ni tuzo uliyostahili. Ni heshima kwa Barcelona kuwa na mchezaji kama wewe”

0 comments:
Post a Comment