Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 October 2014
Sunday, October 26, 2014

Kipa wa Afrika ya Kusini apigwa risasi na kufariki.



  • Na Chikoti Cico
     
    Nahodha na Kipa wa timu ya taifa ya Afrika Kusini anaeichezea pia timu ya Orlando Pirates Senzo Meyiwa apigwa risasi na watu wasio julikana huko Vosloorus karibu na mji Johannesburg katika nyumba aliyokuwa anaishi.

    Taarifa kutoka kwa polisi wa Afrika ya Kusini ambazo ziliandikwa kwenye mtandao wa twitter zilisema “Inabidi tuuvunje utaratibu wa kawaida, tunaweza kuthibitisha kwamba kipa Senzo Meyiwa amepigwa risasi na kufariki wakati anafikishwa hospitalini”

    Katika juhudi za kuwakamata wauaji hao Polisi nchini Afrika ya Kusini wametoa ofa ya kiasi cha randi 150000 sawa na hela za kitanzania 14500000 kama zawadi kwa yeyote atakayetoa taarifa za kusaidia kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo.

    Meyiwa ambaye alianza kuichezea timu ya Orlando Pirates toka mwaka 2006 kabla mauti hayajamkuta aliichezea timu hiyo siku ya Jumamosi dhidi ya Ajax Cape Town na kushinda kwa magaoli 4-1.

    Wakati huo huo timu ya Orlando Pirates ilitoa taarifa kupitia kwa Mwenyekiti wake Dr Irvin Khoza ikisema “Familia ya Orlando Pirates inasikitishwa kwa kifo cha ghafla cha kipa wetu namba moja na nahodha Senzo Meyiwa.

    Hiki ni kifo cha kusikitisha kwa familia ya Senzo na hasa watoto wake, kwa Prlando Pirates na kwa taifa” huku klabu hiyo ikitarajiwa kuongea na waandishi wa habari leo Jumatatu.

    Mpaka mauti yanamkuta Meyiwa alishaichezea timu ya Afrika kusini maarufu kama Bafana Bafana michezo sita huku akipewa unahodha mwezi wa tisa mwaka huu baada ya kuchukua nafasi ya kipa Itumeleng Khune.

    Kifo cha nahodha huyo wa Bafana Bafana linakuwa ni tuko la pili kuikumba nchi ya Afrika Kusini ndani ya wiki moja baada ya karibuni kumpoteza mwanaridha Mbulaeni Mulaudzi aliyefariki kwa ajali ya gari.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!