ZLATAN IBRAHIMOVIC HAKAMATIKI
Kocha wa klabu ya Paris Saint-Germain Laurent Blanc anaamini kuwa,mshambuliaji wake Zlatan Ibrahimovic yuko kwenye msimu wake bora katika maisha ya soka.
Mshambuliaji huyo raia wa Sweeden tayari ameshafunga msimu huu magoli 40 kwenye michuano yote na kuendeleza matumaini yao ya kutetea ubingwa wa ligi yao huko Ufaransa na kusonga mbele kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya ambapo timu hiyo itakutana na Chelsea kutoka Uingereza.
Kocha huyo amabaye ni chezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa anauhakika kuwa,mfungaji wake huyo ambaye amewahi kuzichezea timu za Ac Milan ya Italia na Barcelona ya Hispania,ataendelea kubaki kwenye kiwango chake na hatimaye kuhitimisha mbio zao za kuwania ubingwa wa ligi kwa mafanikio.
"Zlatan ndiye mfungaji wetu namba moja ,ukiangalia rekodi zake ndipo utakapoweza kuthibitisha jamaa ni mzuri kiasi gani." Blanc aliwaambia wanahabari.
"Nina imani kwamba ataendelea kufunga magoli kwenye mechi zetu zote zinazokuja na sioni kwa nini ashindwe kufanya hivyo.
PSG watasafiri na kwenda kuvaana na klabu ya Nice ijumaa ya leo kabla ya kuwakaribisha Chelsea kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwenye mji mkuu wa Ufaransa katikati ya wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment