Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 October 2014
Thursday, October 30, 2014

Pellegrini adai Manchester United ni moto bila Rooney.



Na Rossa Kabwine
 
Meneja wa klabu ya Manchester city, Manuel Pellegrini amesema kuwa wapinzani wao wa jadi timu ya Manchester united, watakuwa hatari bila ya kuepo Wayne Rooney.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza alitarajiwa kurudi katika kikosi cha Manchester united baada ya adhabu yake ya kutumikia kadi nyekundu kuisha wiki hii kwenye mchezo wa derby ya jiji la Manchester utaopigwa kwenye uwanja wa Etihad.

Lakini Ripoti zilizoibuka zinasema kuwa, anaweza kukosa mechi hiyo kutokana na kupata majeruhi mazoezini. Klabu ya Manchester United bado hawajatoa taarifa rasmi ya kumkosa mshambuliaji huyo kuelekea mechi yao na bingwa mtetezi wa ligi kuu Uingereza.

Rooney anashikiria rekodi ya ufungaji magoli mengi katika derby hiyo ya Manchester akifunga magoli 11 katika mechi 22 iliyozikutanisha pambe hizo mbili.

Pellegrini amekataa kuwa timu yake itakuwa na nafuu zaidi kama Rooney atakosekana kwenye mchezo huo “Rooney ni mchezaji muhimu kwa united lakini nadhani mechi kubwa huwa hazitegemei mchezaji mmoja” 

Pellegrin aliongeza kuwa, man united wana wachezaji muhimu watakao tosha kuziba nafasi yake.

Kwa upande mwingine, kocha huyo amethibitisha kurudi kwa kiungo wa timu hiyo Samir Nasri, lakini Frank Lampard hajapona bado kwahiyo, ataikosa mechi hiyo ya derby siku ya jumapili

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!