Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 October 2014
Friday, October 17, 2014

Klopp alia na FIFA/CAF kuhusu Ebola.


Na Chikoti  Cico
 
Baada ya nchi ya Moroco kujitoa kuandaa michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) na kuliomba shirikisho hilo kuahirisha michuano ya AFCON kutokana na ugonjwa wa Ebola.

kocha wa timu ya Borrusia Dortmund Jurgen Klopp ameiomba FIFA na CAF kuwa makini katika kila maamuzi wanayoyafanya kipindi hiki ambacho ugonjwa wa Ebola umekuwa ni tishio barani Africa.

Pamoja na Shirikisho la soka la Afrika CAF kuziomba nchi za Ghana na Afrika ya Kusini kuandaa michuano hii mikubwa kwa nchi za Afrika ambayo itachezwa kuanzia tarehe 17 Januari mpaka Februari 4.

kocha huyo wa Dortmund akihojiwa na waandishi wa habari alisema “naamini mpira hauna maana kwasasa wakati maisha ya watu yakiwa hatarini”

Kocha huyo alisisitiza umuhimu wa ugonjwa wa Ebola kuchukuliwa kwa umakini mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa toka kulipuka kwa ugonjwa huo huko Magharibi mwa Afrika karibu watu 4500 wameambukizwa. 

Wakati huo huo CAF imezifungia nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia kuandaa michezo yoyote ya kimataifa kutokana na kuathirika zaidi na ugonjwa wa Ebola.

Kutokana na taarifa za Shirika la Afya Duniani(WHO) kuhusu usalama na kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa wa Ebola Klopp aliendelea kusema “ nashindwa kuelewa kivipi FiFA ama yeyote anayehusika kufikiri kwamba mipaka yote Afrika ni salama na hakuna mtu yeyote aliyeathirika na Ebola ambaye hataweza kusafiri kwenda nchi nyingine, hata hapa Ulaya hatuwezi kufanya hivyo”

Mwisho kocha huyo kutoka Ujerumani alisema “kama kuna nchi moja ya Afrika ambayo inahisi kwamba haiwezi kuwa mwenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa usalama, basi usalama uwe ni kipaumbele kuliko michuano yenyewe”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!