Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 March 2014
Monday, March 31, 2014

MOURINHO AWATISHIA NYAU PSG

 

Chelsea watakuwa moto wa kuotea mbali kwenye mchezo wa klabu bingwa Ulaya kwenye jiji la Paris huko Ufaransa jumatano hii watakapo wavaa Mabingwa watetezi wa ligi Ufaransa,timu ya PSG.alisema Jose Mourinho. 

Mourinho alikuwa amekasiriki baada ya wachezaji wake ambao wanalipwa mishahara minono kushindwa kuonyesha hali ya kujituma na kujikuta wakipoteza mchezo wao  dhidi ya Crystal Palace kwa kuchapwa bao 1-0.

Mourinho aliwasifia sana mabeki wake bila kuwataja majina na kusema kuwa,muda mwingi wamekuwa wakifanya kazi nzuri huku,akipeleka lawaza zake kwa safu ya ushambuliaji ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikimuangusha katika mbio zake za kupata ushindi dhidi ya timu ndogo.

Mourinho ameeleza kuwa,kitu cha pekee cha kuleta faraja ni wachezaji wote kuhamishia akili na mawazo yao kwenye mchezo wa robo fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya timu ya PSG ambao utafanyika siku ya jumatano huko Paris,nchini Ufaransa.

"Paris ni aina ya mechi ambayo wachezaji wangu watakuwa huru sana kucheza ," alisema. "mechi kubwa, uwanja mkubwa,wapinzani wenye ubora wa kiwango cha juu, watafurahia.watakuwa katika ubora wao kwenye mechi hiyo. Wanaweza kufanya vizuri kwenye mchezo huo"

Mourinho analengo la kuwa kocha wa kwanza kuwahi kushinda kombe  hilo laUlaya  akiwa na klabu 3 tofauti,alifanya hivyo mwaka 2004 akiwa kocha wa Porto na miaka 6 baadae 2010 alipokuwa na Inter Millan.

Mourinho amesema kuwa,mshambuliaji wa Camerron Samwel Eto'o yuko kwenye hatihati ya kuukosa mchezo huo wakati,beki wa kushoto wa Uingereza na timu hiyo,Ashley Cole imethibitika kuwa hatokuwepo kabisa kwenye mchezo huo wa jumatano huko Ufaransa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!