Uchambuzi: Kagera Sugar vs Stand United.
Na Oscar Oscar Jr
Ukiondoa timu ya Ndanda, Kagera Sugar ndiyo timu nyingine ambayo msimu huu haikuwahi kucheza kwenye uwanja wake wa nyumbani. Jumamosi hii watashuka dimbani Kaitaba kuvaana na timu ya Stand United kutoka Mkoa wa Shinyanga.
Kagera Sugar wana elekea kwenye mchezo huo wakiwa kwenye nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kujikusanyia alama tano kutokana na michezo mitatu walioshuka dimbani huku Stand United, wakiwa kwenye nafasi ya nane japokuwa nao wana alama nne. Magoli ya kufunga na kufungwa ndiyo yana watofautisha.
Kagera Sugar msimu huu imeondokewa na wachezaji wake wengi ambao walikuwa nguzo ya timu hiyo akiwemo Themi Felix aliyekuwa mfungaji bora wa klabu hiyo msimu uliopita ambaye amejiunga na Mbeya City.
Ingawa Kagera Sugar hawajaonyesha kuyumba sana, wanatakiwa kupambana na kufanya vizuri mbele ya Stand United.
Matokeo ya Kagera Sugar msimu huu.
Mgambo jkt 1-0 Kagera Sugar
Ruvu jkt 0-2 Kagera Sugar
Polis Moro 1-1 Kagera Sugar
Matokeo ya Stand United msimu huu.
Stand United 1-4 Ndanda fc
Mgambo Jkt 0-1 Stand United
Simba sc 1-1 Stand United
Mchezaji wa kuchungwa kwa upande wa Kagera Sugar
Salum Kanoni ni mchezaji bora kabisa kwa upande wa Kagera Sugar. Ni moja ya wachezaji wachache sana wanaoendelea kucheza vizuri licha ya kuwa aliwahi kucheza klabu kubwa hapa nchini na baadae kutemwa.
Ana uzoefu na ana jua vizuri majukumu yake kama beki. Ana uweza wa kupiga mipira ya adhabu na penati kwa uhakika na hali hii, inamfanya awe miongoni mwa wafungaji wa timu yake.
Mchezaji wa kuchungwa kwa upande wa Stand United.
Salum Kamana ni moja ya wachezaji wanaoonyesha uwezo mkubwa sana dimbani licha ya kuwa bado hana jina kubwa sana. Ukimtazama namna anavyokaba, ubora wa pasi zake na hali ya kujiamini bila shaka ni mtu ambaye atafika mbali sana msimu huu.
Stand United, tofauti na timu nyingine ambazo zinapopata nafasi ya kucheza ligi kuu, hukimbilia kusajili wachezaji wenye majina makubwa ambao huwa wameachwa na timu za Simba na Yanga, wao wamesajili wachezaji kutoka timu nyingi za vijana na kutoka timu za madaraja ya chini ambao bado wanakiu ya mafanikio.
Uwanja wa Kaitaba huwa ni mgumu sana kwa wageni, Stand United maarufu kwa jina la Chama la wana, watakuwa na kibarua kigumu siku hiyo ya Jumamosi. Nani kuibuka na pointi tatu? watu wote wa kanda ya ziwa tukutane kwenye dimba la Kaitaba.
0 comments:
Post a Comment