Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 November 2014
Sunday, November 09, 2014

Liverpool wamestukia dili.


Na Oscar Oscar Jr

Timu ya Liverpool wamejipanga kuhakikisha kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Raheem Sterling haondoki kirahisi. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa kwenye rada za Real Madrid kwa muda mrefu na wababe hao wa Ulaya bado hawajakata tamaa ya kumnasa mchezaji huyo.

Sterling ambaye bado anamkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Liverpool, analipwa mshahara wa Pauni 30,000 huku huduma yake ikionekana kubwa kuliko anachopata. 

Mabosi wa Liverpool wanajiandaa kumpa mkataba mwingine wa miaka mitano ambao utamfanya awe analipwa Pauni 100,000 kwa wiki huku kikiwekwa kipengele cha kumnunu cha Pauni 60M.

Liverpool walifanya mbinu hiyo pia msimu uliopita baada ya timu ya Arsenal kuonekana kumuwinda kwa karibu mshambuliaji, Luiz Suarez ambaye mkataba wake ulikuwa unamruhusu kuondoka kwa kiasi cha fedha kinachozidi Pauni 40M.

Wenger alipeleka Pauni 40M zikakataliwa na kwa mara nyingine, akataka kuongeza Pauni Moja ili kutimiza masharti ya kulipa zaidi ya Pauni 40M kama mkataba ulivyokuwa unazungumza lakini Liverpool, walionekana kumkatalia.

Baadaye, Liverpool waliamua kumuongeza mkataba Luiz Suarez na kuongeza kipengele cha Pauni 75M kwa timu itakayomuhitaji mchezaji huyo ambazo baadaye, zilikuja kulipwa na klabu ya Barcelona ambao walimnunua. 

Raheem Sterling kwa sasa, ni mchezaji anayetegemewa kwenye klabu na timu ya taifa ya Uingereza ambayo inakabiliwa na michuano ya kufuzu kwa michuano ya Euro. Kama kuna timu inamuhitaji, watalazimika kutoa dau la Pauni 60M.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!