Stars yatoka sare na Swaziland.
Na Oscar Oscar Jr
Mchezo wa kirafiki baina ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars dhidi ya Swaziland umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Swaziland ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao mnamo dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza na kufanya timu hizo kumaliza kipindi cha kwanza kwa wenyeji kuwa mbele kwa bao 1-0.
Dakika 45 za kipindi cha pili zilianza kwa timu ya Taifa ya Tanzania kusaka bao la kusawazisha ambalo lilipatikana kupitia kwa mshambuliaji wa klabu ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu kwenye dakika ya 53.
Matokeo haya sio mazuri sana kwa Stars hasa ukizingatia kuwa, Swaziland wako nyama kwa Stars kwenye viwango vya FIFA kwa nafasi 54.
Bado watanzania wameendelea kukosa nafasi ya kushuhudia timu yao baada ya kukosa chombo cha habari hata kimoja ambacho kingeonyesha mchezo huo.
Kuna harakati za kimapinduzi zinapaswa kuchukuliwa ili angalau watanzania waweze kupata fursa ya kuiona timu yao. Kwa Dunia ya leo, ni makosa makubwa sana watu kuendelea kuishi kama wako zama za mawe!
Stars imeshindwa kupata ushindi kwenye mchezo huo licha ya kupata Penalty ambayo, Thomas Ulimwengu alikosa mnamo dakika 72 ya mpambano huo.
Hii ni mechi ya 10 kwa kocha Mart Noij na tayari anaonyesha kushinda michezo mitatu, sare mara nne na Stars imeweza kufungwa mara tatu chini yake.
0 comments:
Post a Comment