Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 December 2014
Friday, December 26, 2014

Kuelekea: JKT RUVU VS RUVU SHOOTING




 Na Oscar Oscar Jr

Mchezo mwingine utakaovuta hisia za wapenzi wa soka hapa nchini ni ule utakao fanyika pale Azam Complex kule Chamazi siku ya leo ambao utawakutanisha JKT RUVU VS RUVU SHOOTING kwenye muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara. 

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 Usiku kufuatia uwanja huo kuwa na taa zinazokidhi vigezo vya mechi kupigwa Usiku.

JKT Ruvu ambao ndiyo wenyeji wa mchezo huo wataingia kwenye mchezo huku wakiwa wanajiamini zaidi baada ya kambi yao ya visiwani Zanzibar kuwa ya mafanikio makubwa. 

JKT Ruvu chini ya kocha Felix Minziro ilifanikiwa kucheza mechi mbili za kirafiki na kushinda mechi zote na wanakata moto huo kuuhamishia kwenye ligi kuu na leo wanaanza na vijana wa Ruvu Shooting wanaoongozwa na kocha Tom Olaba.

Kwa upande wa Ruvu Shooting ambao wanakamata nafasi ya 11 huku wakiwa na alama saba pekee, wanaonekana kupata shida kwenye safu yao ya ushambuliaji ambapo mpaka mzunguko wa saba unakamilika walikuwa wameshafunga mabao manne tu lakini usajili waliofanya, unaonyesha dalili za kutatua tatizo hilo.

JKT Ruvu wao wanaonekana kuwa na mwanzo mzuri wa ligi ambapo mpaka sasa wameshajikusanyia alama 10 na kukamata nafasi ya sita huku wakiwa wametoka sare mara moja, kupoteza michezo mitatu na kushinda mechi tatu.

Endapo vijana wa Felix Minziro wataibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo, wanaweza kupanda hadi kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo kwani watatimiza alama 13 ambazo zimefikiwa na timu za Yanga, Kagera Sugar na Azam na kitakacho watofautisha itakuwa ni tofauti ya magoli pekee.

Ruvu Shooting ambao wameshinda mchezo mmoja pekee, watakuwa wakipambana na ndugu zao hao ili kujiweka sawa kabla ya kurudi kwenye uwanja wao wa mabatini kwa mchezo wao unaofuata dhidi ya Kagera Sugar ambao wanaonekana kuwa kiboko ya vigogo msimu huu kufuatia kuzifunga Simba na Yanga.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!