Diego Costa kucheza mechi dhidi ya QPR
Na Rossa Kabwine
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa akisumbuliwa na majeruhi tangu mwezi wa nane alipojiunga na klabu ya ya Chelsea lakini meneja wake, anatumaini atakuwepo katika mechi ya Jumamosi dhidi ya QPR.
Meneja wa chelsea, Jose Mourihno anategemea Diego Costa na kiungo Ramires watakuwepo katika mechi dhidi nya QPR jumamosi hii. Costa hajacheza tangu alipotoka kutumikia taifa lake katika mechi za kufuzu kwa mataifa ya Ulaya michuano itakayofanyika mwaka 2016.
Wakati mbadala wake Loic Remy nae akiuguza majeraha ya nyonga, mchezaji mkongwe wa klabu hiyo Didier Drogba amecheza mechi zote tangu Remy alipotolewa katika mechi ya klabu bingwa ulaya dhidi ya timu ya Maribor na kufunga magoli matatu.
Tangu aondoke kwenye klabu ya Atletico Madrid na kujiunga na Chelsea, Costa amefunga magoli tisa katika michezo saba aliyocheza na kuifanya Chelsea iendelee kubaki katika nafasi yake ya kwanza katika ligi kuu ya uingereza.
Leo timu ya madaktari wa Hispania walisema kuwa mshambuliaji huyo hakuumia wakati akiwa na timu ya taifa kwenye michezo dhidi ya Slovakia na Luxemburg na hii ni tofauti na kile kocha Jose Mourinho alichosema.
Daktari wa timu ya Hispania, Dr Juan Jose Garcia alikataa na kusema kuwa, Costa alikuwa mzima “Alisema Costa alikuwa mzima na hakusema chochote kuhusu kuumwa na misuli”
Kwa upande wa Ramires, amekuwa hayupo dimbani tangu aumie katika mechi dhidi ya Manchester City wakati timu hizo zilitoka sare yakufungana goli 1-1.
Chelsea itashuka dimbani jumamosi hii kucheza na timu ya QPR katika uwanja wa Stamford Bridge. Chelsea wanaongoza ligi hiyo kwa pointi 23 na watakuwa na wachezaji wao muhimu ambao walikumbwa na mejeruhi.
Kupona kwa ramires na Costa, inaibakiza Chelsea ikisalia na mejeruhi mmoja ambae ni Loic Remy
0 comments:
Post a Comment