Real Sociedad vs Barcelona: saa 5:00 Usiku
Na Oscar Oscar Jr
Barcelona wanatarajiwa kushuka dimbani usiku wa leo kumenyana na timu ya kocha wa zamani wa Manchester United, David Moyes timu ya Real Sociedad amabao wanakamata nafasi ya 14 huku wakiwa na alama 15 pekee. Mchezo huo utapigwa majira ya saa 5:00 Usiku.
Real Sociedad wameonekana kuwa wagumu sana kufungwa pindi wanapocheza na Barcelona kwa miaka ya hivi karibuni hasa wanapokuwa nyumbani lakini kuondoka kwa mshambuliaji kama Antoine Greizmann, kumemuacha Carlos Vella akiwa hana mtu wa kushirikiana nae kwa kiasi kikubwa ili kufunga magoli mengi.
Washambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na Neymar ambao licha ya kurejea kikosini wakiwa wamechelewa, bila shaka watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza mchezo huo kutokana na umuhimu wa mchezo wenyewe na hasa baada ya Atletico Madrid kushinda mchezo wao wa jana na kulingana alana na Barcelona (38).
Lionel Messi ambaye ameshafunga mabao 15 ya La Liga msimu huu, bila shaka ataungana na Neymar ambaye amefunga magoli 11 kuhakikisha kwamba wanaondoka na alama tatu na kuongeza presha kwa Real Madrid ambao wako kileleni wakiwa na alama 39.
Real Madrid nao leo watakuwa wakipambana na timu ya Valencia ugenini japo wana mchezo mmoja pungufu ukilinganisha na Barcelona kabla ya kwenda kuwavaa Atletico Madrid wiki ijayo kwenye kombe la Mfalme.
Mwendo wa kocha David Moyes akiwa na Real Sociedad bado ni wa kusua sua kwani bado hajaonyesha kiwango kizuri licha ya kuwa timu hiyo chini yake kutopoteza mchezo wowote wakiwa nyumbani.
Leo atakuwa na shughuli pevu mbele ya vijana wa Luiz Enrique ambao wanataka kufuta machungu ya kumaliza msimu uliopita bila kunyakuwa taji lolote.
Real Sociedad ambao wameshinda mechi tatu pekee, watakawa na kibarua cha kuwanyima alama tatu Barcelona ambao wameshinda mechi 12 msimu huu kati ya mechi 16 walizokwishacheza..
0 comments:
Post a Comment