Searching...
Image and video hosting by TinyPic
14 August 2014
Thursday, August 14, 2014

Roberto Martinez aongeza wanajeshi wanne.



 Na Oscar Oscar Jr

Klabu ya Everton ambayo msimu uliopita ikiwa chini ya kocha Roberto Martinez ilifanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya tano huku ikifunga mabao 61 na kuruhusu wavu wake kutikiswa mara 72, imeendelea kujiimarisha kwa kumsajili Mshambuliaji Romelo Lukaku kutoka Chelsea kwa uhamisho wa kudumu na kumchukuwa winga Christian Atsu kwa mkopo msimu mzima.

Mghana huyo wa miaka 22 huenda akacheze mechi yake ya kwanza wakati wa mechi ya kufungua msimu wa ligi dhidi ya Leicester City Jumamosi ya kesho. 

Atsu alikuwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Ghana ambacho kilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani kwenye fainali za kombe la dunia zilizomalizika mwezi julai mwaka huu.



Atsu ndiye mchezaji wan ne kuchukuliwa na Everton kipindi cha kuhama wachezaji baada ya straika Romelu Lukaku, pia kutoka Chelsea, kiungo wa kati wa zamani wa Uingereza Gareth Barry na kiungo wa kati Mbosnia Muhamed Besic kujiunga na timu hiyo ya jijini Liverpool. 


Atsu alianza uchezaji wake Ureno akiwa na Porto kabla ya kujiunga na Chelsea 2013.
Alikaa msimu uliopita katika klabu ya Uholanzi ya Vitesee kwa mkopo Arnhem na alianza mechi zote tatu za Ghana katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!