Man United majanga tena!
Na Oscar Oscar Jr
Timu ya Man United iliweza kufungwa mabao 43 msimu uliopita huku safu yake ya ulinzi ikitawanyika baada ya msimu kumalizika. Rio Ferdinand, Patrice Evra na Nahodha wao Nemanja Vidic wote kutimka kwenye maskani ya klabu hiyo yenye mafanikio makubwa Uingereza pale Old Trafford.
Moja kati ya usajili uliofanyika ni pamoja na kumleta Luke Shaw kutoka Southampton ili aje kuziba nafasi iliyoachwa na Patrice Evra ambaye ametimkia kwenye ligi kuu ya nchini Italia.
Kulikuwa na habari za kocha wa United Loius Van Gaal kutoridhika na mwenendo wa beki huyo lakini, kabla hata ya kuanza kwa ligi tayari Shaw ameripotiwa kuumia.
Mchezaji mpya wa Manchester United Luke Shaw atakosa mwanzo wa Ligi ya Premia na huenda akae nje wiki nne baada ya kupata jeraha la paja, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo.
Mkabaji huyo wa kushoto wa umri wa miaka 19, alitua Old Trafford akitokea Southampton Juni kwa takriban £30 milioni, na bado hajachezea United mechi yake ya kwanza ya ushindani.
Shaw, aliyekuwa kwenye kikosi cha Uingereza cha Kombe la Dunia na aliyechezea taifa mara ya tatu mechi iliyoisha sare tasa dhidi ya Costa Rica, alikosa mechi ya mwisho ya kirafiki ya United ya kujiandaa kwa ligi Jumanne dhidi ya Valencia.
Huenda akalazimika kusubiri mwezi kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza ya ushindani na meneja mpya wa United Louis van Gaal anajikuna kichwa kufuatia kuondoka kwa mkabaji wa kushoto mwenye tajriba Patrice Evra aliyehamia Juventus.
United wataanza kampeni yao Ligi ya Premia kwa mechi dhidi ya Swansea City uwanjani Old Trafford Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment