Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 August 2014
Sunday, August 10, 2014

Ndugu wa damu ndani ya Kagame leo.


 Na Oscar Oscar

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Azam inatarajia kujitupa uwanjani leo hii kumenyana na ndugu zao timu ya KMKM kutoka Zanzibar kwenye mchezo wao wa pili wa kuwania nafasi ya kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Kagame linaloendelea huko nchini Rwanda.

Azam na KMKM zote zilishindwa kupata matokeo ya ushindi baada ya kujikuta wote wakitoka sare michezo ya kwanza. Pamoja na mchezo mzuri waliouonyesha Azam bado walishindwa kupata bao mbele ya wenyeji Rayon Sports ya Rwanda huku KMKM nao wakishindwa kutamba mbela ya Atlabara ya Sudani Kusini.

Azam ambayo ilifanikiwa kufunga mabao 51 kwenye ligi kuu bara msimu uliopita, ilikuwa inaongezwa na Kipre Tchetche kwenye safu ya ushambuliaji ambaye alifunga mabao 13 ya ligi, Mcha Hamisi mwenye mabao matano na John Bocco mwenye mabao saba. 

Pamoja na kumuongeza kipindi cha pili Didier Kavumbagu aliyefunga mabao 11 akiwa na klabu ya Yanga, bado azam haikuweza kufunga bao.

Ushindi wa yoyote kati ya kmkm au azam, utamfanya mmoja awe kwenye hali ngumu kuelekea kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo Rwanda amepewa nafasi za kupeleka timu tatu huku Burundi ikiwa na timu mbili.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!