Na Oscar Oscar Jr
Golikipa wa kabu ya Mtibwa Sugar, Said Mohamed atakuwa na kibarua kigumu sana langoni kuhakikisha anaisaidia timu yake kutoruhusu mabao mengi kutinga wavuni kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo waliweza kuruhusu mabao 30 kutinga langoni
Kipa huyo ameweza kuchukuwa nafasi ya kwanza kwenye kikosi cha wakatamiwa hao wa Turiani Morogoro baada ya aliyekuwa kipa namba moja Hussein Sharrif maarufu kama Cassilas kujiunga na wekundu wa Msimbazi timu ya Simba.
Mtibwa Sugar ni moja kati ya timu ambazo hazionekani kuimarika kwa misimu ya hivi karibuni huku moja ya sababu ikiwa ni kuruhusu mara kwa mara wachezaji wake muhimu kuweza kutimka klabuni hapo. Mbali na Cassilas kutimka, kiungo Shabaan Kisiga pia ameondoka.
Mtibwa Sugar walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-0 mbele ya timu ya Azam siku chache zilizopita lakini bado imekuwa ni vigumu kwa mashabiki wake kuamini kama timu hiyo inauwezo tena wa kurudia mafanikio ambayo waliyapata mwaka 1999 na 2000 ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara mara mbili mfululizo.
0 comments:
Post a Comment