Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 August 2014
Sunday, August 10, 2014

Arsenal kutamba leo mbele ya Man City?



 Na Oscar Oscar Jr

 Baada ya timu ya Chelsea kumaliza msimu uliopita ikiwa timu yenye safu bora ya ulinzi baada ya kuruhusu mabao 27 pekee, Manchester City waliibuka kuwa timu yenye safu bora ya ushambuliaji baada ya kufunga mabao 102.

Leo majira ya jioni kutakuwa na mpambano wa Ngao ya jamii ambao unawakutanisha mabingwa wa kombe la FA timu ya Arsenal dhidi ya mabingwa wa ligi kuu timu ya Manchester City kwenye dimba la Wembley.


Arsenal kwa miaka ya hivi karibuni, imekuwa ni timu amabayo  haifanyi vizuri hasa kwenye michezo wanayokutana na timu zinazotawala nne bora kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza. Arsenal walipoteza mchezo wa ligi dhidi ya Man City ugenini kwa kufungwa mabao 6-3 huku wakipata sare ya 1-1 nyumbani.

Katika mechi za majaribio ambazo timu ya Arsenal imeshiriki ikiwa ni pamoja na kombe lao Emirates , wameonekana kuwatumia wachezaji wao waliowasajili na wameonekana kufanya vizuri isipokuwa Alexies Sanchez na huenda leo akawa na nafasi ya kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo kutoka London.

Matokeo mazuri kwa arsenal leo inaweza kuwa ishara nzuri kuelekea kufungulia kwa pazia la ligi kuu kwa sababu pamoja na kutwaa ubingwa wa FA msimu uliopita, bado mashabiki hawana imani kubwa juu ya timu yao.

kutwaa ubingwa wa ligi kuu na ule wa Ulaya msimu huu inaweza kuwa zawadi kubwa sana ambayo wamekuwa wakiisubiri kwa muda mrefu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!