Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 December 2014
Monday, December 29, 2014

Benchi la ufundi la Yanga linapaswa kufanya mabadiliko.


Na Samuel Samuel 
0652464525

Kocha msaidizi wa Stand United, Emmanuel Masawe akiwa kocha mkuu wa timu hiyo mzunguko wa kwanza alitamka jambo moja kabla ya kupokea kipigo cha 3-0 toka kwa miamba hao wa soka wa zamani Tanzania. 

" kuifunga Yanga si jambo rahisi kutokana na mfumo wa safu ya ulinzi ya timu hiyo. Ni mabeki wanaoelewana sana na wamekaa kwa muda mrefu" Hakuwa mbali na ukweli kocha huyo.

Ukimtazama Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Mbuyu Twite na hata Juma Abduli kuna uwiano mzuri wa kiuchezaji lakini ukuta huu unaanza kugeuka chujio kwa haraka. 

Tatizo walimu wote waliopita Yanga, wameitengeneza back line hiyo katika mgongo wa Nadir Haroub . Amegeuka kiranja mkuu wa idara hiyo. Yeye ndiye mwenye uwezo mkubwa kuliko wote. 

Uwezo wa kuwapanga wenzake, kusahihisha makosa yao na hata kuwakemea pale wanapokosa umakini. Sasa inapotokea Nadir hayupo , ukuta mzima unageuka yatima. 

Wakianza kushambuliwa vichwani wanapiga picha taswira ya Nadir ! Wanatamani kusikia sauti yake. Ukitaka kujua ubora wa Yondani ni pale anapofanyiwa back up na Nadir. Tactically, Yondani ana makosa mengi sana. 

Uchezaji wa rafu na kuchelewa kufanya clearance au kuziba njia za mipira kabla washambuliaji wa kati wa timu pinzani hawajaiona. 

Naamini kama Nadir angekuwa uwanjani juzi angemfokea Mrwanda na kumwambia kama kiungo mkabaji shuka chini kumsaidia Manyama ambaye alikuwa na makosa mengi. 

Sasa spana za benchi la ufundi chini ya Pluijm ziifungue hii dhana ya kumtegemea Nadir na kuwatengeneza mabeki wote kujiamini na kutekeleza majukumu yao independently. 

Back line itengenezwe kuweza kuwa na partnership na mchezaji yoyote yule. Spana zimwangalie kwa jicho la karibu Yondani na Dida. Kuna sehemu zimelegea.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!