Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 August 2014
Monday, August 11, 2014

Kumtimua Loga ni sawa ila muda haukuwa muafaka.



 Na Oscar Oscar Jr

 Jana Rais wa Simba Evance Aveva alitangaza kusitisha mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Zdravko Logarusic kwa kile kilichodaiwa kocha huyo kushindwa kwenda sambamba na tamaduni za timu hiyo.

Uamuzi huo umekuja baada ya siku kudhaa viongozi hao wa klabu ya Simba kumpatia mkataba mpya kocha huyo baada ya ule wa awali kuwa umemalizika. Kuvunja mkataba maana yake ni kwamba timu inaingia gharama za kulipa fidia lakini, klabu hii huwa haioni tabu yoyote kufanya hivyo kwa sababu hasara sio tatizo kwao. 

Wakati Simba walipokuwa na sababu ya msingi ya kumtimua kocha Logarusic kufuatia matokeo mabovu msimu uliopita, wao hawakufanya hivyo na wakaona ni vema kumpa mkataba mpya! Loga katika mechi 13 za mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara, alifanikiwa kuambulia alama 14 pekee ambazo ni sawa na wastani wa alama moja kwenye kila mechi.

Wakati Logarusic ametuliza presha na kuanza kuisuka timu yake kwa ajili ya msimu ujao, wao wamemtimua! makocha wazawa hawaaminiki na wageni hali ni ile ile!! 


Logarusic anaweza kuwa moja ya makocha bora na mtu mwenye uwezo wa kuipa timu mafanikio lakini kwa muda alioiongoza Simba, ameshindwa kuthibitisha hilo.

Simba wanaweza kuwa sawa kwa kumtimua Loga lakini haikuwa muda muafaka. Hali ya utata wa maisha ya kocha huyo kwenye mitaa ya Msimbazi iliingia nyongo baada ya timu hiyo kuchezea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa timu ya Zesco United kwenye mechi ya kirafiki siku ya Simba day.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!