Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 August 2014
Friday, August 15, 2014

Crystal Palace bila kocha mkuu mbele ya Arsenal



 Na Cicoti Jr

Tony Pulis ameng’atuka kuifundisha timu ya Crystal Palace baada ya kinachosemekana kutokuelewana na Steve Parish kwenye maswala mazima ya uendeshaji wa klabu haswa swala la usajili wa wachezaji. 

Katika kikao cha masaa 6 kilichofanyika kati ya Pulis na Mwenyekiti wa Crystal Palace kujadili usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu 2014/2015 kikao kilichopeleka Tony Pulis kukubali kwa hiari kuachia ngazi hasa baada ya Mwenyekiti wake kugoma kufanya usajili wa wachezaji kama Gylfi Sigurdsson, Steven Caulker and Michu ambao Pulis aliwahitaji ili kuimarisha maandalizi ya msimu mpya wa ligi kwa timu ya Crstal Palace. 

Baada ya kumaliza nafasi ya 11 kwenye msimu wa ligi wa 2013/2014 Tony alihitaji kufanya usajili zaidi ili kuimarisha kikosi cha Crystal Palace lakini Steve Parish hakuwa tayari kufanya usajili mkubwa ambao ungegharimu pesa nyingi kutoka kwenye bajeti ya timu ya Crystal Palace. 

Kung’atuka kwa Pulis kunapelekea timu ya Crystal Palace kufunguza pazia la ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal ikiongozwa na Dave Kemp aliyekuwa kocha msaidizi wa Tony Pulis ambaye pia ataondoka baada ya mechi hiyo.

Upande wa pili, kuna taarifa zinazosema kocha wa zamani wa Cardiff City Malky Mackay anaweza kupewa nafasi ya kuiongoza Crystal Palace kwenye msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!