Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 August 2014
Saturday, August 16, 2014

Loius Van Gaal apewa lawama



Na Oscar Oscar Jr

Taarifa zilizotoka kufuatia kuumia kwa mlinzi wa Manchester United Luke Shaw zinzelezwa kusababishwa na mazoezi ya kocha wa timu hiyo Louis van Gaal ambaye ameongeza muda wa kufanya mazoezi na idadi tofauti na ilivyokuwa hapo awali., amebainisha kocha msaidizi wa zamani wa Wales Raymond Verheijen.

Mkabaji huyo wa kushoto wa Uingereza, aliyejiunga na United kutoka Southampton kipindi cha kuhama wachezaji kwa pauni 30 milioni ($50.06 milioni), huenda akakaa nje mwezi mmoja kutokana na tatizo la misuli ya paja na bila shaka atakosa mwanzo wa ligi wakiwa nyumbani dhidi ya Swansea City leo mchana.

Verheijen alimtaja Mholanzi mwenzake Van Gaal (LVG) kuwa "kocha sahihi” wa United lakini akamshutumu meneja huyo wa zamani wa Uholanzi kwa “kutojua kazi” na kuwafanyika wachezaji wake mazoezi kupita kiasi. 

Inaelezwa hata kuelekea michuano ya kombe la Dunia ambapo Loius Van Gaal aliiongoza Uholanzi kumaliza kwenye nafasi ya tatu, majeruhi ya wachezaji wake ya mara kwa mara yalichangiwa na mazoezi makali na yanafanyika zaidi ya mara moja kwa siku.

Verheijen alidokeza pia kuwa ni vigumu kwa wasaidizi wa Van Gaal kuweza kumshauri na akawaelewa kutokana na misimamo yake mikali. 

Mara nyingi wamejikuta wakikubali kila anachosema bosi huyo ambaye leo ataiongoza Manchester United kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya timu ya Swansea City katika dimba la Old Trafford.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!